Huduma ya sala kwaajili ya

siku ya Kimataifa ya kutafuta Amani bila mapigano

Tarehe 2 oktoba 2009

Tarehe 2 Oktoba 2009 ni siku maalum kwa watu wote duniani hasa wale wengi wetu wanaojitotolea kuishi habari njema ya amani, haki na upatanisho.Ni kumbukumbuku ya kuzaliwa kwake Mahatma Gandhi, aliyesaidia India kupata uhuru na kuvipatia vyama mwamko wa haki na uhuru dunia kote. Siku ya Kimataifa ya kutafuta haki bila fujo ilikubaliwa na nchi 192 za Jumuia ya Umoja wa mataifa wakati wa mkutano mkuu mnamo tarehe 15 mwezi wa sita mwaka 2007.

Unaalikwa kushiriki kwa njia ya sala hii pamoja na wanataasisi wenzako, .tunahamasisha pia matumizi ya sala hii maparokiani,mashuleni,Vyuoni,katika Vyuo Vikuu na katika huduma nyingine za Shirika lako. Tunakualika ili uweze kutuma hii sala kwa wafanyakazi wenzako na hata wale mnaotoa huduma pamoja.